Umuhimu wa elimu katika Uislamu
کد: 249916 تاریخ: 1390/00/00منبع: print

Umuhimu wa elimu katika Uislamu


 Umuhimu wa elimu katika Uislamu

 

Katika Uislamu elimu na masomo yamepewa umuhimu mkubwa sana. Aya ya kwanza ya Quran Tukufu imesisitiza kuhusu elimu na masomo na umuhimu wa kalamu. Umuhimu huu ni mkubwa kiasi kwamba Uislamu unasema ni faradhi au lazima kwa Muislamu mwanaume na mwanamke kutafuta elimu. Riwaya za Kiislamu pia zinamuusia mwanaadamu kutafuta elimu na masomo hadi kwenye maeneo ya mbali zaidi duniani.
Mbali na hayo, Uislamu unasema utafutaji elimu unapaswa kuendelea katika kipindi chote cha maisha ya mwanadamu. Mtume Mtukufu wa Uislamu SAW anasame: "Tafuteni elimu kutoka susu hadi kaburini."
Moja ya sababu ambazo zimepelekea Uislamu kuzingatia sana suala la elimu ni hii kuwa elimu hufungua milango ya ujuzi na kumuwezesha mwanaadamu kupata maarifa zaidi kumuhusu Mwenyezi Mungu.
Kwa mtazamo wa Uislamu, kujifunza sayansi zinazohusiana na haja na mahitaji ya mwanaadamu ni jambo la dharura na wajibu. Elimu inayofaa ni ile ambayo inahudumia jamii ya wanaadamu na inastawisha amani, urafiki na maadili ya kibinaadamu. Kwa mtazamo huu wasomi na wanazuoni waliotangulia walijipatia elimu katika mazingira magumu sana ili kuhakikisha kwamba elimu na sayansi zinazomfaa mwanaadamu zinaenea.
Ayatullahil Udhma Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anasema hivi kuhusu uhusiano wa kupata elimu na ustawi wa nchi: "Kwa hakika nchi ambayo haina uwezo wa kupata elimu haiwezi kuwa na uwezo, uhuru kamili, utambulisho, usalama wala kuwadhaminia wanainchi maisha bora. Elimu katika maisha ya mwanaadamu ni jambo ambalo linampa nguvu"
Utafiti kuhusu sayansi za kimaumbile hasa taaluma ya fizikia ni jambo ambalo huleta ustawi wa jamii ya mwanaadamu na pia husaidia kuhusu uvumbuzi wa baadhi ya masuala ya kweli kuhusu dunia. Utafiti kama huu unaweza kutusaidia katika kujifahamu na vile vile kusaidia katika kufahamu ulivyoumbwa ulimwengu.
Fizikia ni sayansi inayohusu maumbile ya dunia, ambayo inahusu asili ya viungo vya ulimwengu. Ni taaluma kutoka shina la sayansi yenye kushughulika na maada na uhusiano wake na nishati. Jitihada za Wanafizikia zimepelekea kugunduliwa kanuni nyingi kama vile za kujifunza kuhusu baadhi ya matukio ya kimaumbile. Ingawa mafanikio yaliyopatikana ni machache yakilinganishwa na yale asiyoyajua mwanaadamu, lakini jitihada za pande zote na za kasi za wasomi zinatoa matumaini kuwa mwanaadamu anaweza kuvumbua siri nyingi za maumbile.
Wasomi bingwa Wairani
Tunaweza kumtaja mwanafizikia maarufu Muirani ambaye pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Princeton Marekani, Profesa Ali Yazdani kuwa kati ya wasomi bingwa wa fizikia ambao wamechukua hatua mpya katika ustawi wa sayansi.
Jarida la kisayansi duniani la Popular Science limemtaja Profesa Yazdani kuwa kati ya wasomi bingwa kumi bora zaidi duniani. Ameorodheshwa katika toleo la mwaka 2008 la jarida hilo.
Jarida hilo limemtaja Profesa Ali Yazdani kuwa mbunifu wa kile kilichotajwa kuwa "ndoto ya atomiki". Ubunifu huo unajumuisha microscope iliyo kama bomba yenye ukubwa wa meza ya kawaida ya ofisini ambayo kazi yake ni kuchunguza kiwango cha joto katika vipitisho vya juu vya umeme. Chombo hiki kina uwezo wa kupunguza kiwango cha joto hadi sufuri. Kupitia mfumo huu, Profesa Yazdani amefanikiwa kwa mfululizo kufuatilia atomu moja katika kipindi cha miezi kadhaa. Profesa Yazdani alianza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Berkeley California katika uga wa mekaniki ya quantum baada ya kuhamia Marekani. Alipata cheti cha PHD katika chuo Kikuu cha Stanford mwaka 1995. Alikuwa naibu profesa wa mekaniki katika Chuo Kikuu cha Illinois kutoka mwaka 1997 hadi 2005 na tokea wakati huo hadi sasa amekuwa akihadhiri katika Chuo Kikuu cha Princeton. Ripoti kuhusu mafanikio ya kipekee ya Profesa Yazdani yamechapishwa pia katika jarida la Science and Nature. Mark Jannot Mhariri wa Jarida la Popular Science anasema hivi kuhusu Profesa Yazdani: "Jarida letu linatoa shukrani kwa wanasayansi hawa ambao wamevumbua siri za dunia kwa upeo wa kina"
Miaka miwili iliyopita, Maryam Mirzakhani mhadhiri kijana Muirani katika Chuo Kikuu cha Princeton ambaye alipata shahda ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Shariff mjini Tehran ni kati ya wasomi Wairani walioiletea nchi fakhari katika olympiadi ya Fizikia. Bi. Mirzakhani ametambuliwa na jarida la Popular Science kuwa kati ya wasomi bora zaidi wa mwaka.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepata nafasi maalumu miongoni mwa wanafizikia katika taaluma ya sayansi ya kimsingi hasa fiziki na hivyo kuwa miongoni mwa nchi bora katika olympiadi za fizikia.
Bw. Ja'afar Mehrdad, Mkuu wa Kituo cha Sayansi na Teknolojia cha Iran anasema hivi kuhusu uzalishaji sayansi katika taaluma ya fizikia: ‘Uzalisahji wa Iran mwaka 2007 katika uga wa fizikia ulikuwa wa makala muhimu 2,986 na yametajwa kama marejeo mara 12,800 jambo ambalo ni la fakhari kwa taifa la Iran"
Hebu tuzingatie hapa mahojiano ya Amir Abbas Salarkia kijana msomi bingwa wa Iran ambaye sasa ana umri wa takribani miaka 21 na ambaye alishinda medali katika Olympidia ya 39 ya Kimataifa ya Fizikia huko Vietnam. Kuhusu mafanikio makubwa ya vijana wa Iran, Salarkia anasema: "Vijana Wairani ni werevu, mahiri na wadadisi mahiri hasa katika uga wa fizikia. Mtu wa kwanza duniani kufanya utafiti kuhusu kanuni za kuvunjika nuru alikuwa Muirani aitwaye Haytham. Ibn Haytham alipima uhusiano wa mwangaza na kuakisiwa kwake hadi nyuzi 80. Baadaye wasomi wa Ulaya akiwemo Descartes waligundua ukweli huu kupitia maandishi ya Ibn Haytham".
Salarikia anaamini kuwa kuna wasomi bingwa wengi Wairani ambao wanapaswa kuarifishwa duniani.
Amir Abbas Salarkia sasa anasoma uhandisi wa umeme katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Shariff.

 
ایمیل:
نام:
پیام:
کد امنیتی را در کادر وارد کنید
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  آخرین عناوین