Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Israel ikiishambulia kijeshi Iran itajuta kwani jibu la uchokozi huo litakuwa kali
Namba: 261892 Tarehe: 1390/00/00Rejea: print

Israel ikiishambulia kijeshi Iran itajuta kwani jibu la uchokozi huo litakuwa kali

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, endapo utawala wa Kizayuni wa Israel utaishambulia kijeshi Iran basi utajuta kwa hatua yake hiyo kwani jibu la Tehran kwa uchokozi huo litakuwa kali. 

 Israel ikiishambulia kijeshi Iran itajuta kwani jibu la uchokozi huo litakuwa kali
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, endapo utawala wa Kizayuni wa Israel utaishambulia kijeshi Iran basi utajuta kwa hatua yake hiyo kwani jibu la Tehran kwa uchokozi huo litakuwa kali. Rais Ahmadinejad amebainisha kwamba, anaioinya Israel isithubutu kuanzisha chokochoko ya aina yoyote ile dhidi ya taifa hili; kwani itajuta kwa hatua yake hiyo. Dakta Ahmadinejad amesema, Iran inakaribisha mno kuundwa nchi huru ya Palestina na kwamba, hatua hiyo inapaswa kuwa utangulizi wa kukombolewa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni maghasibu. Rais wa Iran ameongeza kwamba, madola ya eneo hili la Mashariki ya Kati hayapaswi kuruhusu madola ya Magharibi yaje na kuwa na satwa na udhibiti na kwamba, Iran inawataka wananchi wa eneo hili kuwa macho na kutoukubali uingiliaji wa kigeni katika masuala yao ya ndani. Kuhusiana na suala la Quds, Rais Ahmadinejad amesema, suala hili sio suala la Iran au la nchi za Kiarabu tu, bali kadhia ya Quds ni kadhia ya ulimwengu mzima wa Kiislamu.
 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani