| Namba: 266870 | Tarehe: 1390/00/00 | Rejea: IQNA | print |
QUR'ANI Qur'ani Nchini Iran |
Ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul Bayt(a.s)-ABNA- Ikimnakili Kijana aliyehifadhi Qur’ani Tukufu nchini Iran amesema kuhifadhi Qur’ani hakupaswi kumzuia mwenye kufanya hivyo kuendeleza masomo yake ya kawaida ya ‘kiakademia’ .
Mohammad Mahdi Haghgooyan amesema katika mahojiano na Radio Qur’an mjini Tehran kuwa: "Nilianza kuhifadhi Qur’ani nikiwa na umri wa miaka minane na kuhifadhi Qur’ani kikamilifu nikiwa na umri wa miaka 10. Niliendelea na masomo yangu hadi chuo kikuu na sasa natarajia kuanza masomo ya Shahada ya Uzamili (M.A) katika taaluma ya Qur’ani na Sayansi za Hadithi katika Chuo Kikuu cha Tarbiat Modaress mjini Tehran".
"Kuhifadhi Qur’ani hakujawa kizingiti katika masomo yangu wala shughuli za kimichezo. Nilikuwa nikitumia masaa mawili kwa siku kuhifadhi Qur’ani".