| Namba: 268993 | Tarehe: 1390/00/00 | Rejea: Ripoti ya ABNA | print |
Historia ya waja wema Imam Kadhim(a.s) |
Yeye ni Imam Mussa bin Jaafar Al-kaadhim (a.s) na mama yake ni Hamidah Al-muswaffah, alizaliwa (a.s) katika sehemu iitwayo (Ab’waa) nayo ni sehemu iliyoko kati ya Makka na Madina siku ya juma pili tarehe (7) mwezi wa Safar mwaka (128) hijiria na aliiaga Dunia akiwa na umri wa miaka (55) kwa kulishwa Sumu na kufa shahidi katika jela ya Haroun baada ya kumfunga kwa muda mrefu kwa muda wa miaka (14) kwa dhuluma na uadui, na alifariki siku ya Ijumaa tarehe (25) ya mwezi wa Rajab mwaka (183) na mwanae Imam Ridhaa (a.s) kusimamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika mahala lilipo kaburi lake tukufu kwa hivi sasa katika mji wa Kaadhimiyyah huko Iraq.
Na Imam alikuwa ndie mwenye elumu zaidi kati ya watu wa zama zake na mbora wao na mkarimu zaidi kati yao na shujaa zaidi na amwenye tabia njema, mwenye umbile bora na mororo, mwenye kudhihiri juu yake fadhila, elimu na mwenye hadhi tukufu, mwenye kufanya sana ibada na mwenye kurefusha sijda zake, na kutokana na kuvunja kwake ghadhabu na kuto kasirika akaitwa Al-kaadhim, na kutokana na wema wake na utukufu wake alikuwa akiitwa Al-abdus swalih (mja mwema).
Na kutokana na elimu yake nyingi aliweza kudhihirisha elimu za aina tofauti, elimu ambazo ziliwashangaza watu, na kati ya elimu hizo ni hadithi ya (Burayha) mkuu wa Wakiristo alie mashuhuri alie shindwa na Imam na kukosa la kusema mwishowe kusilimu na kuwa muislaam safi.
Na miongoni mwa ukarimu wake (a.s) ni kuwa fakiri mmoja alimuomba Dinari mia moja na Imam kwa kutaka kumjaribu akamuuliza mas'ala au swali moja ili kujua kiwango cha maarifa yake, yule fakiri alipo jibu mas'ala yale Imam akampatia Dinari elfu moja.
Na Imam (a.s) alikuwa ni mwenye sauti nzuri sana pindi anapo soma Qur'ani na alikuwa ni mfanya ibada sana kati ya watu na kusoma sana Qur'ani, na alikuwa ni mwenye kurefusha sana sijda na rukuu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na mwenye kulia sana na mwenye mazingatio, na alifikiwa na shahada hali ya kuwa yuko kwenye hali ya kusujudu (yaani akiwa ni mmwenye kusujudu).