Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Madina kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Mbinu Bora ya Kuchapisha Qur'ani
Namba: 270614 Tarehe: 1390/00/00Rejea: Ripoti ya ABNAprint

Qur-ani
Madina kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Mbinu Bora ya Kuchapisha Qur'ani

Kituo cha kuchapisha na kusambaza Qur'ani Tukufu cha Mfalme Fahad katika mji mtakatifu wa Madina kitakuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Mbinu Bora ya Kuchapisha Qur'ani Tukufu. 

 Madina kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Mbinu Bora ya Kuchapisha Qur

Ripoti ya ABNA- Kwa sasa kituo hicho cha kuchapisha Qur'ani kinachunguza mipango ya kuitisha kongamano hilo ambalo litafanyika katika siku chache zijazo.

Watu, taasisi, vyombo rasmi na visivyokuwa rasmi vinavyojishughulisha na masuala ya Qur'ani kutoka nchi mbalimbali vitaalikwa kushiriki katika kongamano hilo. Kongamano hilo litajadili na kuchunguza tafiti na tajiriba za washiriki katika medani ya uchapishaji wa Qur'ani Tukufu.

Katibu Mkuu wa Kituo cha Kuchapisha Qur'ani cha Mfalme Fahad Muhammad Salim bin Shadid al Aufi amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kukutanisha pamoja wanaharakati wa masuala ya uchapishaji Qur'ani kutoka nchi mbalimbali kwa ajili ya kupasisha sheria, kanuni na mbinu bora zinazokubalika na pande zote kwa ajili ya kuchapisha Qur'ani Tukufu, sheria ambazo zitatekelezwa kote duniani.

Amesema kuwa kongamano hilo ni katika juhudi za kuzuia uchapishaji wa nakana za Qur'ani zenye makosa ya kimaandishi.

 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani