Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Harakati za kuteka Wall Street kuendelea Marekani
Namba: 272537 Tarehe: 1390/00/00Rejea: IRNAprint

Muamko wa Kiislamu
Harakati za kuteka Wall Street kuendelea Marekani

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Washington nchini Marekani amechunguza na kujadili mwenendo wa harakati ya kuteka nyara Wall Street na taathira zake katika uchaguzi ujao wa rais na kusisitiza kuwa hapana shaka kuwa harakati hii itakuwa na taathira katika kubadili hali ya sasa nchini Marekani. 

 Harakati za kuteka Wall Street kuendelea Marekani

Ripoti ya ABNA- Kituo cha habari cha Klewtv kimeripoti kuwa T.V Read mtaalamu wa harakati za kijamii na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Washington amesema kuwa malalamiko ya wananchi wa Marekani yatakuwa na taathira kubwa kwani kama inavyoshuhudiwa sasa mazungumzo na maamuzi yanayohusiana na masuala ya uchumi hapa nchini yamebadilika, na hii ni moja ya malengo muhimu ya harakati ya kuteka nyara Wall Street.

Mhadhiri huyo wa Marekani ameongeza kuwa katika harakati ya sasa kunashuhudiwa mshikamano mkubwa kati ya vijana na jumuiya za wafanyakazi kiasi kwamba nishati kubwa ya vijana na itibari na uungaji mkono wa jumuiya za wafanyakazi vitabadilisha mlingano wa kiuchumi nchini Marekani.

 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani