Mahakama hiyo imedai kwamba licha ya kuwa picha za video zilizoonyeshwa kupitia mtandao wa intaneti na mhalifu huyo Ernesto Rojas Abbate zilikuwa za kukera na za kichochezi, lakini eti hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kwamba alikusudia kuchochea hisia za ubaguzi, chuki au vitendo vya ghasia dhidi ya Waislamu.
Baada ya mahakama hiyo kutoa hukumu hiyo wakili wa mhalifu huyo mbaguzi amejigamba na kudai kwamba madai ya kukosewa heshima matukufu ya kidini hayapasi kutolewa katika nchi ya kisekula na isiyozingatia mafundisho ya kidini katika uendeshaji wa mambo yake kama vile Ufaransa.
Rojas Abbate alitiwa nguvuni na polisi ya Strsbourg baada ya Waislamu kulalamikia vikali hatua yake ya kuonyesha kitendo hicho kichafu dhidi ya Qur'ani Tukufu katika mkanda wa video. Kitendo hicho cha dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu kilifanywa na mbaguzi huyo mwezi Oktoba mwaka uliopita.
Licha ya kuwa mwendesha mashtaka wa Strasbourg alikuwa ametaka mahakama itoe kifungo kisicho na maana cha mhalifu huyo kusalia nyumbani kwa muda wa miezi mitatu na kutozwa faini ya euro 1000, lakini mahakama ya rufaa imeharibu zaidi mambo kwa kufutilia mbali moja kwa moja mashtaka yaliyokuwa yakimkabili mhalifu huyo