ABNA inatuarifu kuwa: mlima Kilimanjaro ambao ni wa kwanza kwa urefu barani Afrika na wapili kwa urefu Duniani uliopo kaskazini mwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.ambapo mlima huo si tu kwamba ni fahari ya Tanzania bali Afrika kwa ujumla pia ni kivutio na changa moto ya utalii kwa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla umekosa nafasi y akuingizwa kwenye maajabu saba ya dunia baada ya wa Afrika mashariki hasa watanzania kutotuma meseji za kutosha kuupitisha mlima huo katika kinyang'anyiro hicho adhimu.
msemaji wa taasisi ya New Seven Wonders ambayo ndio mratibu wa kinyang'anyiro hicho cha upigiaji kura wa vivutio 28 vilivyoingia fainali amesema kuwa:upigaji hafifu wa kura kutoka Tanzania ndio sababu kuu ya mlima huo kukosa nafasi hiyo adhimu.
yafaa kuashiria kuwa asilimia 95 ya kura za mlima huo zilitoka Marekani na ulaya hata hivyo hazikutosheleza na kusababisha mlima huo wa kihistoria kukosa nafasi na badala yake kuchukuliwa na Meza(Table Mountain) uliopo katika jiji la Cape Town Afrika kusini.