Akihutubia hii leo mjini New York Marekani pambizoni mwa Mkutano wa Kamati ya 3 ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Muhammad Javad Larijani ameongeza kwamba, madai yanayotolewa na Marekani na washirika wake kwamba Iran inavunja haki za binadamu ni sehemu ya siasa za Washington katika eneo hili. Aidha Larijani amesema Marekani haina nia ya kuimarisha demokrasia bali lengo lake ni kufuatilia maslahi yake haramu katika njia ambazo zinakwenda kinyume na demokrasia katika eneo la Mashariki ya Kati. Mkuu wa Baraza la Haki za Binadamu la Iran aidha ameashiria kushiriki Marekani katika vitendo kadhaa vya kigaidi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kueleza kwamba, Washington inaunga mkono makundi ya kigaidi kama vile Tondar, Rigi na Mujahedin Khalq na kusema kuwa hiyo ni mifano ya wazi inayoonyesha jinsi Marekani inavyokiuka haki za binadamu.