Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Ukatili dhidi ya Waislamu waongezeka Marekani
Namba: 279118 Tarehe: 1390/00/00Rejea: ABNAprint

Athari za Muamko wa Kiislamu
Ukatili dhidi ya Waislamu waongezeka Marekani

Takwimu zilizotolewa na polisi ya FBI nchini Marekani zinasema kuwa kiwango cha jinai na ukatili unaofanywa dhidi ya Waislamu nchini humo kimeongezeka kwa asilimia 50 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. 

 Ukatili dhidi ya Waislamu waongezeka Marekani

Gazeti la Nation limeripoti kuwa ripoti ya FBI inaonyesha kwamba, kwa mfano tu jinai na uhalifu unaosababishwa na chuki dhidi ya Waislamu umeongezeka kutoka kesi 107 mwaka 2009 hadi 160 mwaka 2010.

Pamoja na hayo takwimu hizo haziakisi ukweli wa mambo kuhusu ukatili na jinai zinazofanywa dhidi ya Waislamu nchini Marekani, kwani polisi ya FBI huwa hairipoti mambo yote yanayotokea.

Wataalamu wa mambo wanasema kuwa sehemu moja ya ongezeko la ukatili na jinai dhidi ya Waislamu ni matokeo ya hotuba na matamshi yanayotolewa na wanasiasa na makundi yenye misimamo mikali ya Marekani dhidi ya Uislamu likiwemo kundi la "Stop Islamization of America.

 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani