Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Uchambuzi wa kufungwa ubalozi wa Uingereza Nchini iran
Namba: 281515 Tarehe: 1390/00/00Rejea: ABNAprint

Siku ya ghadhabu Tehran
Uchambuzi wa kufungwa ubalozi wa Uingereza Nchini iran

Ubalozi wa Uingereza mjini Tehran siku ya Jumanne ulikuwa medani ya maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu waliokuwa wakilaani hatua hasimu na za uingiliaji kati za Uingereza dhidi ya Iran. Hata kama kwa mtazamo wa sheria za kidiplomasia katika uga wa kimataifa matukio ya Jumanne yanaweza kukosolewa na taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia ilikosoa yaliyojiri, lakini huu ni upande moja tu wa sarafu. 

 Uchambuzi wa kufungwa ubalozi wa Uingereza Nchini iran

Serikali ya London imechochea propaganda za vyombo vya habari na maazimio ya Umoja wa Ulaya na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika kile kinachotajwa ni kulaani matukio ya Jumanne katika ubalozi wa Uingereza mjini Tehran. Uingereza ina historia ndefu ya misimamo hasimu dhidi ya Iran. Kuhusu hatua ambazo kwa kawaida zinapaswa kuchukuliwa katika kulinda ofisi za kidiplomasia kwa mujibu wa sheria za kimataifa , Iran ni muhanga wa kukiukwa haki zake za kimataifa kwani ubalozi wa Iran mjini London ulishambuliwa Aprili 30 mwaka 1980. Hili faili linaweza kufunguliwa na kuanza kuchunguzwa upya kwa kutegemea ushahidi uliopo.
Aprili mwaka 1980, magaidi sita ambao walidaiwa kufika London kutoka Baghdad walishambulia kwa silaha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini London na kuwashikilia mateka watu 26 kwa muda wa siku sita. Katika tukio hilo la kigaidi, wanadiplomasia wawili wa Iran , Abbas Lavasani na Ali Samadzadeh waliuawa shahidi. Hii ni katika hali ambayo baadhi ya duru zinadokeza kuwa kuuawa watekaji nyara katika oparesheni ya jeshi la Uingereza ndani ya Ubalozi wa Iran ni jambo lililoibua shaka na utata mkubwa. Weledi wa mambo wanasema kuwa, kwa kuuawa magaidi hao, habari muhimu walizokuwa nazo kuhusu utekaji nyara huo zilitoweka. Ushahidi uliopo unaonyesha kuwa iwapo serikali ya Uingereza haikuwa mratibu mkuu wa nyuma ya pazia katika hujuma dhidi ya ubalozi wa Iran mjini London, bila shaka inabeba lawama ya hujuma hiyo ya kigaidi. Isisahaulike kuwa serikali ya Uingereza ilikua na wajibu wa kudhamini usalama wa ubalozi huo. Sasa serikali ya London imeanzisha hujuma ya kisiasa dhidi ya Iran na kujaribu kuonyesha kuwa eti imedhulumuwa. Hii ni katika hali ambayo taifa la Iran katika vipindi mbali mbali vya historia limedhulimiwa na utawala wa kibeberu wa Uingereza. Kwa hivyo hatua ya hivi karibuni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran kuhusu kupunguza kiwango cha uhusiano wa kidiplomasia na Uingereza ni radiamali ya matakwa ya taifa la Iran. Hatua ya bunge la Iran inakuja baada ya hatua hasimu za Uingereza katika siku za hivi karibuni. Wakuu wa London katika kufuata kibubusa tabia hasimu za Marekani dhidi ya Iran, walitoa madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran . Madai hayo ni kuhusu njama ya kumuua balozi wa Saudia nchini Marekani, madai ya ukiukaji haki za binaadamu na madai kuhusu shughuli za nyuklia za Iran zenye malengo ya amani . Aidha Uingereza imeidhinisha vikwazo vya upande moja dhidi ya Iran na hivyo kuwasha mtoto mpya wa fitina. Natija ya hatua hizo hasimu za Uingereza ni kuibua hasira zya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iran. Wanafunzi hao walikuwa wakiandamana kwa mnasaba wa mwaka wa pili tokea alipouawa shahidi mwanasayansi wa nyuklia wa Iran ambaye alilengwa na magaidi wa mashirika ya kijasusi ya Mossad la Israel, CIA la Marekani na MI6 la Uingereza. Ikumbukwe kuwa siku moja baada ya kuuawa kigaidi wanasayansi wawili wa nyuklia nchini Iran, gazeti la Independent la Uingereza liliandika kuwa kuuawa Dkt. Shahryar kulikuwa natija ya oparesheni ya pamoja ya Mossad, CIA na MI6 kwa lengo la kuchelewesha mpango wa nyuklia wa Iran. Itakumbukwa kuwa Novemba 29 mwaka 2010, vibaraka wa mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi walitekeleza hujuma ya kuwauwa wasomi wa ngazi za juu wa vyuo vikuu hapa nchini. Katika tukio hilo Dkt. Majid Shahryari mwanachama wa jopo la kisayansi la Chuo Kikuu cha Shahid Beheshti alikufa shahidi. Naye mwenzake, Dkt. Feridoun Abbasi, ambaye sasa ni Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran, alijeruhiwa akiwa na mke wake katika hujuma hiyo ya kigaidi. Aidha Januari mwaka 2009 Dkt. Masoud Ali Mohammadi msomi Muirani wa Chuo Kikuu cha Tehran aliuawa katika hujuma ya kigaidi ambayo pia iliungwa mkono na madola ya kibeberu hasa Uingereza na Marekani. Sasa swali ambalo tunauliza hapa ni hili, je, ni kwa nini Baraza la Uslama linachukua hatua ya haraka kulaani kuingia wanachuo wa Iran katika ubalozi wa Uingereza Tehran lakini inanyamazia kimya makusudi hatua hasimu za Uingereza dhidi ya Iran?

 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani