Mfanyakazi wa zamani wa Shirika la Upepelezi la Marekani FBI amesema kuwa Marekani na Nato wanayapa mafunzo makundi yanayobeba silaha ya Silaha huko katika mji wa Hakkari kusini mashariki mwa Uturuki. Sibel Edmond amesema, amepokea taarifa kutoka Uturuki na katika duru za Marekani zinazoonyesha kuwa utoaji mafunzo kwa makundi ya upinzani ya Syria yanayoongozwa na Kanali Riad al Assad kulianza mwezi Mei mwaka huu. Mfanyakazi huyo wa zamani wa FBI ameongeza kuwa Marekani inahusika katika kuingiza silaha huko Syria kutoka katika kambi ya kijeshi ya Incirlik huko Uturuki ili kuyasaidia makundi hayo yanayobeba silaha huko Syria.