Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Matokeo ya uchaguzi nchini Ufaransa na Ugiriki yaleta wasiwasi EU
Namba: 313829 Tarehe: 2012/05/09 - 03:29Rejea: Abna.irprint

Nini kitakacho tokea Barani Ulaya baada ya kuangushwa Sarkozy?!
Matokeo ya uchaguzi nchini Ufaransa na Ugiriki yaleta wasiwasi EU

Wikiendi iliyopita, Wafaransa wamemchagua rais mpya, na nchini Ugiriki pia ulifanyika uchaguzi wa wabunge ambao ni wa kwanza kufanyika tangu nchi hiyo ikumbwe na msukosuko mkubwa wa madeni. Uchaguzi huo umeleta wasiwasi kwa wanasiasa wa Umoja wa Ulaya na viongozi wa nchi wanachama wa umoja huo kuhusu maendeleo ya kushughulikiwa msukosuko wa madeni. 

 Matokeo ya uchaguzi nchini Ufaransa na Ugiriki yaleta wasiwasi EU

Ujerumani ni nchi yenye wasiwasi mkubwa zaidi na matokeo haya ya uchaguzi wa
rais nchini Ufaransa. Kwani katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili iliyopita
toka msukosuko wa madeni uzikumbe Nchi za Ulaya, Ujerumani ilikuwa
ikishirikiana na Ufaransa katika kutekeleza sera za kubana matumizi katika nchi
za wanachama wa Umoja wa Ulaya. Ujerumani ina wasiwasi kwamba, kushindwa kupata
awamu nyingine ya urais kwa Nicolas Sarkozy kutasababisha kuvunjika kwa
ushirikiano huo kati ya Ufaransa na Ujerumani, na Nchi zengine za wanachama wa
Umoja wa Ulaya zinaweza kupunguza nguvu ya kutekeleza sera za kubana matumizi
na kuleta  mageuzi ya kiuchumi, na hata kuziweka kando.
Tumeshuhudia kuwa toka mwanzoni mwa mwaka huu, Umoja wa Ulaya ulianza
kurekebisha sera zake za kiuchumi, yaani kutoa kipaumbele kwa lengo la kuhimiza
ongezeko la uchumi. Tangu msukosuko wa madeni utokee barani Ulaya, wanasiasa wa
Umoja wa Ulaya walikuwa wanatatizwa na kuweka uwiano kati ya kubana matumizi na
kuhimiza ongezeko la uchumi. Kutoka na matatizo ya madeni, nchi za Ulaya
zililazimika kuchukua hatua za kubana matumizi, lakini pia zina wasiwasi kwamba
hatua hizo zinaweza kukwamisha ongezeko la uchumi. Hivi sasa inaonekana
wasiwasi huo umebadilika kuwa hali halisi. Kubana matumizi kupita kiasi
kumefanya uchumi barani Ulaya urudi katika hali ya kudidimia na idadi ya watu
wasio na ajira kuendelea kuongezeka. Umoja wa Ulaya unatunga mkakati wa
kuchochea ongezeko la uchumi ambao unatarajiwa kupitishwa kwenye mkutano wa
wakuu utakaofanyika mwezi Juni. Hata hivyo Ujerumani haifurahii maoni hayo na
haipendi sera za sasa za kubana matumizi ziachwe.


 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani