Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Je! Siku zijazo Nchi ya Bahrain yaweza kuwa Mkoa wa 14 wa Saudia Arabia?
Namba: 315002 Tarehe: 2012/05/14 - 04:24Rejea: Abna.irprint

Muamko wa Kiislamu
Je! Siku zijazo Nchi ya Bahrain yaweza kuwa Mkoa wa 14 wa Saudia Arabia?

Siku ya leo Viongozi wa Nchi za Persian Gulf wamekutana Riadh Mji Mkuu wa Saudia Arabia kujadili jinsi ya kubadili Uongozi wa Nchi hizo mbili mbazo za kabiliwa na upinzani mkali, pia kujadili nini la kufanya ili kukabili upinzani Nchini Bahrain na kusimamisha maandamano ya amani Nchini humo. 

 Je! Siku zijazo Nchi ya Bahrain yaweza kuwa Mkoa wa 14 wa Saudia Arabia?

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Siku ya leo Saudia Arabia imeweka kikao cha usaliti wa Nchi ya Bahrain na Wananchi wake kwa kuitaka serikali na utawala wa Kifalme kukubali maombi ya Saudia Arabia kifanya Bahrain kuwa Mkoa wa Saudia Arabia, kikao na suala hili lilipingwa na walokuwa wengi hasa Wananchi wa Saudia Arabia na Bahrain.Sheikh Ali Salmaniy Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Wafaq- Jumuiya ambayo inawafuasi wengi- alisema: kuzungumzia suala la kuifanya Bahrain kuwa moja ya Mkoa wa Saudia Arabia hatukubaliani nalo kwani Wananchi wa Bahrain kamwe hawakubaliani na suala hili, na tunaiomba serikali na utawala haramu wa Kifalme wa Alikhalifa uheshimu matakwa ya Wananchi wa Bahrain, kikao hiki ni kusababisha na kuamsha hasira za Wananchi kwani utawala Bahrain kamwe hauheshimu Wananchi, na hili suala ni siasa ya kijinga ya utawala, utawala lazima utaulizwa kwa kile kitakachotokea baada ya kikao hicho.

Akisema: si Bunge wala Mawakilishi wa Nchi hakuna alieomba na kupitisha suala hilo, na makubaliano na hatua yoyote ile itakayo chukuliwa katika kikao hicho ni batili na haito zingatiwa.

Uamuzi wa utawala wa Saudia Arabia na Bahrain ni kuzuiya harakati ya kila aina Nchini Bahrain na kukabiliana na wapinzani wa Nchi hiyo.Uamuzi huu ni ishara ya kushindwa utawala wa Alikhalifa na kuadia siku za mwisho wake, kwani waandamanaji wa Bahrain wameonyesha Ulimwengu kuwa maandamano yao ni ya amani.

Uongizi wa Nchi za Persian Gulf siku ya Jumaatatu utakutana Mji Mkuu wa Saudia Arabia Riadh kuzungumzia Umoja huo ”Uongozi wa Nchi za Persian Gulf”  kuwa Muungano badala ya umoja, suala hilo litafanya Nchi ndogo ndogo za Kiarabu kama Bahrain, Qatar,Emirat na Kuwait kuwa chini ya Uongozi mmoja, ila lengo la kuunda Muungano huyo ni kuitaka Nchi ya Bahrain kuwa chini ya Saudia Arabia.

 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani