| Namba: 316330 | Tarehe: 2012/05/20 - 05:03 | Rejea: CRI | print |
Mamia ya wapalestina kupambana na Jeshi la Israeli |
Mamia ya wapalestina jana walipambana na wanajeshi wa
Israeli mashariki mwa Jerusalem walipokuwa wakiandamana kuadhimisha siku ya
"Nakbah". Nakbah ni siku ambayo nchi ya Israeli ilianzishwa na
kusababisha wapalestina kupoteza makazi yao. Licha ya usalama kuimarishwa,
maandamano ya mwaka huu hayakuwa na vurugu nyingi ikilinganishwa na miaka ya
nyuma ambapo vurugu zilishuhudiwa karibu na lango la Damascus na makazi ya
Etzion kusini mwa Jerusalem. Hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa kwenye makabiliano
hayo.