Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Waasi wa Tuareg watafuta suluhu na Ansar Dine
Namba: 319418 Tarehe: 2012/06/02 - 19:01Rejea: Dwprint

Waasi wa Tuareg watafuta suluhu na Ansar Dine

Waasi wa Tuareg na viongozi wa kundi la Kiislamu kaskazini mwa Mali wanajaribu kupunguza kupata muafaka, baada ya Watuareg kuukataa mpango wa kuanzisha taifa lililojitenga na Mali lenye kufuata Sharia 

 Waasi wa Tuareg watafuta suluhu na Ansar Dine





Viongozi wa Vuguvugu la Tuareg la Ukombozi wa Azawad
(MNLA) na wale wa kundi la Ansar Dine walikutana katika mji wa kaskazini
mashariki wa Gao hapo jana (Ijumaa, 1 Juni 2012) baada ya MNLA kusema kwamba
imeachana na mpango wa makubaliano yaliyodumu kwa wiki moja kwa sababu kundi la
Ansar Dine kusisitiza utumiaji wa Sharia.



Walil Ag Cherif wa Ansar Dine ameiambia Shirika la Habari
la AFP kwa njia ya simu kuhusiana na mazungumzo hayo kwa njia ya simu bila ya
kutaja undani wake. Mkutano huo umethibitishwa kufanyika na upande wa Tuareg.
Ansar Dine (Walinzi wa Imani) walikuwa wamekataa kubadilisha msimamo wao wa
kutumia mfumo wa Sharia, na ambao ulikataliwa na kundi la MLNA.



"Uongozi wa kisiasa wa MNLA ulipingana na msimamo wa
Ansar Dine kutumia Sharia katika Azawad na kubakia na azimio lake la
kutochanganya dini na siasa, unakataa makubaliano ya tarehe 26 Mei 2012
uliofanya na kundi hilo na unatangaza chochote kuhusiana na makubaliano hayo
kimefutwa," ilisema taarifa ya MLNA.



Tamko la Alhamis lililosainiwa na mwanachama wa ngazi ya
juu wa MNLA, Hamma Ag Mahmoud katika mji mkuu wa Azawad, Gao, lilikuwa la
mwanzo rasmi kuthibitisha kujitoa kwa waasi hao kwenye makubaliano na Ansar
Dine.



Makundi hayo hasimu, ambayo yaliiteka miji mikuu
kaskazini mwa mwali baada ya mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 22 Machi katika mji
mkuu, Bamako, yana itikadi na malengo tafauti na mahusiano yao yamekuwa ya
mashaka.



Mgawanyiko wa MNLA na Ansar Dine



Dhamira iliyodumu muda mchache ya kuyaunganisha ilikufa
haraka kutokana na hamu ya Ansar Dine kulazimisha utawala wa sharia katika dola
hilo mpya, ambalo hadi sasa halitambuliki kimataifa.



Msemaji wa MLNA anayeishi mjini Paris, Mossa Ag Attaher, aliiambia
Afpa kwamba walikuwa wamekubali wazo la kuwa na Dola ya Kiislamu "lakini
ilipaswa kuandikwa kwamba tutatekeleza Uislamu usio wa misimamo mikali na wenye
ustahmilivu, bila ya kutaja sharia. Hatuko tayari kujikuta sisi wenyewe
tumefungwa na sharia kutoka siku hadi siku," aliongeza.



Lakini ambapo MLNA ilikuwa tayari kupambana na ugaidi,
alisema Watuareg hawatowacha dhamira yao ya kuwa na dola huru ya Azawad, jina
wanalotumia kwa nchi kaskazini mwa Mali, ambalo ni eneo kubwa zaidi kuliko nchi
nzima ya Ufaransa. Tayari waasi wa Tuareg wameshapoteza wapiganaji wengi kwa
Ansar Dine.



Mgawanyiko ndani ya MNLA



Chanzo kimoja cha usalama kwenye eneo hilo, akizungumza
kwa sharti la kutokutajwa jina, aliiambia AFP kwamba kujiunga na Ansar Dine
kumewagawa waasi wa MLNA, ambao wengi wao walirudi kwenye eneo hilo mwezi
Januari wakiwa na silaha nzito kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muammar
Gaddafi, na kufufua mapambano yao ya muda mrefu ya kudai uhuru.



Waasi hao waliwasukuma wanajeshi wa serikali kutoka
kaskazini mwa nchi hiyo na kupelekea mapinduzi yaliyoiondoa serikali ya Mali,
baada ya maafisa wa jeshi kulalamika kwamba walikuwa hawapati vifaa
walivyohitaji kupambana.



Katika kulitumia ombe la kisiasa, waasi hao walifanikiwa
kuchukuwa udhibiti wa eneo la kaskazini la nchi hiyo ambalo ni karibuni nusu
nzima ya Mali. Lakini kundi la Ansar Dine, linaloungwa mkono na tawi la
al-Qaida katika eneo la Sahel (AQIM), walichukuwa udhibiti wa mapambano hayo,
kwa kuichukua miji muhimu yote kama vile Timbuktu na kuanzisha sharia ya
Kiislamu.



Viongozi
wa eneo hilo la mataifa ya magharibi wamekuwa wakihofia kwamba dola
iliyojitenga na Mali kaskazini mwa nchi hiyo inaweza kuwa ngome imara ya
al-Qaida. Tayari kiongozi wa juu wa AQIM amewashauri Ansar Dine kuunda dola la
Kiislamu.







 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani