Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Marekani yawasha moto Nchini Syria
Namba: 319963 Tarehe: 2012/06/05 - 01:30Rejea: print

Marekani yawasha moto Nchini Syria

Marekani inatumaini kuwa Russia itaiwekea shinikizo serikali ya Syria, ili kuhimiza mabadiliko ya utawala nchini humo. 

 Marekani yawasha moto Nchini Syria

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Hilary Clinton ameeleza hayo wakati alipoongea kwa simu na waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov. Bw. Lavrov amesisitiza kuwa, mgogoro wa Syria unapaswa kutatuliwa kwa njia ya amani na mazungumzo, pamoja na juhudi za muda mrefu za pande zote, kama ilivyofanyika wakati wa kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Yemen.

Wizara ya mambo ya nje ya Russia imesema, Russia inalaani vikali mauaji yaliyotokea hivi karibuni huko Houla nchini Syria, lakini haikubaliani na azimio la Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji hayo, kwani linawakilisha maoni ya Baraza hilo pekee. Russia ina wasiwasi kuwa, mauaji hayo yanatumiwa na baadhi ya nchi kuhujumu mpango wa amani uliopendekezwa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu kuhusu mgogoro wa Syria Bw Kofi Annan
 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani