Taamir Amar mmoja kati ya viongozi wa ofisi ya vijana katika kikundi chama cha Uhuru na Uadilifu nchini Misri amesema Shafiq anahusika katika umwagaji damu wa waandamanaji, katika tukio la uvamizi wa wapanda ngamia (mamluki wa Mubaraka) kuwavamia waandamanaji katika midani ya Tahariri, nae kipindi hicho akiwa ni waziri mkuu wa utawala huo wa kidekteta.
Pia aliongeza kusema kuwa viongozi wote waloshiriki katika mauaji ya waandamanaji ndio wafanya kambeni wakubwa upande wa Ahmad Shafiq.
Mwisho alisema Muhammad Mirsi si mgombea wa kikundi cha Ikhwanul Muslimin tu bali ni mgombea wa wanamapinduzi wote.