Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Mazungumzo ya Pakistani na Marekani ya kwama
Namba: 321706 Tarehe: 2012/06/12 - 17:37Rejea: print

Mazungumzo ya Pakistani na Marekani ya kwama

Maafisa wa serikali wa Marekani wanarudi nyumbani baada ya mkutano wao na wawakilishi wa serikali ya Pakistan wa kuitaka Pakistan kufungua tena mpaka wake na Afganistan ili kuruhusu majeshi ya NATO na vifaa vyao majeshi hayo kupitia katika mpaka wao kwenda Afgansitan kutozaa matunda.

 

 Mazungumzo ya Pakistani na Marekani ya kwama

Kukwama kwa mazungunzo hayo yanahatarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia kati ya Washington DC na Islamabad, baada ya mazungumzo hayo kuvunjika katika kipindi cha wiki sita za mashauriano.

Pakistan ilifunga mpaka wake mwezi Novemba mwaka uliopita ili kuzuia majeshi ya NATO kuendelea kutumia mpaka huo kusafirisha vifaa vyao hadi nchini Afghnaistan wanakolinda usalama na kupambana na kundi la kigadii la Taliban.

Pakistani ilichukuwa hatuwa hii baada, baada ya majeshi ya NATO kutekeleza shambulizi la anga katika mpaka huo na kusabibisha mauaji ya wanajeshi 24 wa Pakistan, tukio ambalo NATO ilisema lilitekelezwa kwa makosa.

Uhusiano wa nchi hizi mbili uliendelea kudhoofika zaidi wiki iliopita pale kamanda wa majeshi ya Pakistani alikataa kumpokea kwa mazungumzo kiongozi nambari mbili wa majeshi ya Marekani, ambae alisafiri kutoka Marekani kwa ajili ya kujadili na viongozi wa pakistani kuhusu mzozo huo.

Serikali ya Islamabad imeweka ngumu zaidi katika kupandisha maradufu kiwango kilichokuwa kikitozwa kwa kila lori inayoingia kupitia njia hiyo, jambo ambalo linapelekea NATO kuendelea kutumia ndege zake katika kusafirisha vifaa vyake, na njia hi yaonekana kuwa ghali zaidi.

Washington imeondowa wajumbe wake kwenye mazungumzo na pakistani, lakini imesema wanachukuwa mapunziko kidogo, mazungumzo yataendelea.

 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani