| Namba: 322498 | Tarehe: 2012/06/16 - 09:40 | Rejea: abna | print |
Mama na Mtoto wakumbatiana baada ya ugomvi wa miaka 20 |
Ripoti ya Shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Imeelezwa kuwa katika Kijiji cha Isfarain Nchini Iran Mama na Mtoto wake wa Kike walikumbatiana baada ya ugonvi wa miaka 20 bila kuongea, yote hiyo ni baraka ya Itikafu ya Mwezi Mtukufu wa Rajab.
Sheikh Hamzah Peiravi alisema: Itikafu ni mfano wa Ibada ya Hija ina amali tofauti kama Swala, Swaumu, kusoma Qur`ani, Dua, Dhikr na kutawasali kwa Mwenye enzi Mungu na Mtume wake(saw) na watu wa Nyumbani kwake.
Sheikh Hamzah katika maongezi yake na Kitengo cha Tabligh cha Mkoa wa Khurasan Nchini Iran alisema: Imam Baqir (as) amesema: Mwenye kuwa katika Itikafu anusi uturi(Pafyum) na hataladhadhi kwa vyenye harufu nzuri, na habishani, na hanunuwi wala kuuza.
«المُعْتَکِفُ لا یَشَمُّ الطِّیبَ وَ لا یَتَلَذَّذُ بِالرَّیْحَانِ وَ لا یُمَارِی وَ لا یَشْتَرِی وَ لا یَبِیعُ.»
Akiendelea kusema Sheikh Hamzah: Itikafu ya Mwaka huu ilikuwa ni yenye baraka kuthibiti hilo ni tukio muhimu katika ibada hii kwa kukumbatiana Mama na Mtoto wake wa kike baada ya ugonvi wa miaka 20 bila kutoleana salam wala kujuliana hali, na hii ni ishara ya kuonyesha umuhimu Ibada na athari zake kwa Mwanadamu.