Na haya ni madhumuni ya ujumbe huo: Amani iwe juuyenu nduguzangu wamisri na wale wananchi ambao wanasherehekea ushindi wa Muhammad Mirsi katika viwanja vya tahriri kwa ushindi wa urais nchini Misri, lakini mimi nashangaa saana kwamba kitugani kinachowafurahisha mpaka mwafurahi kiasi hiki?.
Nadhani munafikiri kwamba kumchagua huyu bwana mwenye mandevu usoni na mwenye kuitakidi kuwa(utawala wa kiislamu ndio utatuzi wa matatizo yenu ) haliyakuwa hamufahamu suala hilo limebeba ujumbe gani kwa wananchi?
Ivi munafikiria kuna umuhimu saana kujikurubisha na Iran na kujitenga na wamarekani na wagharibi? ivi munaona ni muhimu sana kwenu kujiunga na magaidi(Iran) na kikundi cha Hamasi na vyengine vya kigaidi, ni fikra mbaya munayofikiri, achini fikra hizo ili kuokoa uchumi wenu usianguke. …
Maneno haya yanaashiria kuawa Israil na wamarekani wanatishika sana kunako fungamano la Misri na Iran kwani wanafahamu malengo ya Iran ni umoja wa kiislamu na na utakapopatikana umoja wa kiislamu hawataweza kuwatisha waislamu.