| Namba: 327960 | Tarehe: 2012/07/09 - 20:11 | Rejea: ABNA.ir | print |
Kofi Annan awasili nchini Syria kujadili mpango wa amani |
Awali Annan aliliambia gazeti moja la Ufaransa kuwa, juhudi za jumuiya ya kimataifa za kukomesha hali ya vurugu nchini Syria iliyodumu kwa miezi 16 hazijafanyikiwa. Amesema tofauti kati ya nchi za kanda hiyo pamoja na zile kati ya nchi kubwa duniani zinafanya hali ya nchini Syria izidi kuwa mbaya. Ameshauri kwamba Iran inaweza kutoa mchango katika kutatua mgogoro wa Syria.