| Namba: 328440 | Tarehe: 2012/07/11 - 19:15 | Rejea: ABNA.ir | print |
Muamko wa Kiislamu Kufariki Mashia wa 2 Saudia Arabia |
Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- imeeleza kuwa Maelfu ya watu kuandamana Nchini Saudia Arabia kupinda vitendo vya utawala Saudia Arabia kwa kumtia mbaroni Mwanazuoni maarufu wa Nchi hiyo Sheikh Namr, na katika maandamano hayo kuliuawa watu 2 kwa kupigwa risasi, maandamano hayo yametokea mashariki mwa Saudia Arabia.

Ripoti zimeeleza kuwa watu walouawa ni Sayyid Akbar Shaakhuri kutoka Mkoa wa Al-Awamia, na Sayyid Muhammad Filfil kutoka Mkoa wa Qatif.
Imeelezwa kuwa lengo la maandamano hayo ni kupinga vitendo vya utawala wa Ali Saudi kwa kushika Wanazuoni wa Nchi hiyo bila sababu za msingi, pia ripoti zaeleza kuwa ili kutawanyisha waaandamanaji vikosi vya usalama vya Saudia Arabia vilitumia silaha baridi, na hawakutosheka kwa hilo walitumia risasi ili kutawanyisha waandamanaji na kusababisha kuuwa watu wa 2 katika waandamanaji hao.
Aidha imeelezwa kuwa vikosi vya usalama vya Saudia Arabia vilivamia Basi la Ayatullah Sheikh Namr A`ali Namr na kupelekwa sehemu isofahamika, vikosi hivyo vilitumia risasi kusimamisha Gari la Ayatullah Sheikh Namr.

Ayatullah Sheikh Namr alizaliwa mwaka 1959 katika Mkoa wa Al-awalia na Baba yake alikuwa mwazuoni maarufu wa mkoa huo, Ayatullah Sheikh Namr ni maarufu katika Mkoa wa Al-awamia na Qatif. Pia sio mara kwanza kushikwa Shekh kitendo km hicho kimeshatokea mara nyingi.