| Namba: 329061 | Tarehe: 2012/07/14 - 19:01 | Rejea: ABNA.ir | print |
Polisi nchini Tanzania kumshika mkenya mmoja aliemteka Daktari nyara |
Kamanda wa polisi mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova amemtaja Joshua Gitu Mhindi mwenye umri wa miaka 31 na kuongeza kuwa amekutwa na hati ya kusafiria inayothibitisha uraia wa mtu huyo ambaye tayari jalada la kesi yake limekabidhiwa kwa mwendesha mashtaka wa serikali ya Tanzania.
Kiongozi wa chama cha madaktari nchini Tanzania alitekwa nyara,kuteswa na kutupwa nje kidogo ya jiji la Dar es salaam mwezi wa sita na watu ambao hawakufahamika,na kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu nje ya Tanzania.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi nchini humo limepiga maandamano ya madaktari yaliyopangwa kufanyika siku ya jumatatu 16 mwezi huu.