Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Kofi Anan: Viongozi wa Nchi za Kimaghari hawakuonyesha ushirikiano kutatua mgogoro wa Syria
Namba: 334097 Tarehe: 2012/08/03 - 18:37Rejea: ABNA.irprint

Kofi Anan: Viongozi wa Nchi za Kimaghari hawakuonyesha ushirikiano kutatua mgogoro wa Syria

Kofi Anan baada ya kujiuzulu katika madaraka ya kutatua mgogoro wa Syria alieleza kuwa: Baadhi ya Viongozi wa Kimagharibi hawakuonyesha ushirikiano wao kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Syria na kupuuzia baadhi ya mambo.

 

 Kofi Anan: Viongozi wa Nchi za Kimaghari hawakuonyesha ushirikiano kutatua mgogoro wa Syria

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Kofi Anan alijiuzulu baada ya kuona baadhi ya Viongozi wa kimagharibi kupuuzia njia sahihi za kutatua mgogoro wa Syria, na alieleza kuwa; Viongozi wa Kimagharibi hawakuonyesha ushirkiano kutatua mgogro wa Syria na kuchukuwa zisizokuwa sahihi.

Aidha alisema: Kutaka baadhi ya Nchi kuongeza idadi ya Majeshi na kupewa Silaha waasi ni moja katika sababu ya kufelisha njia sahihi za kutatua mgogoro wa Nchi ya Syria, kuthibitisha hilo ni Mkutano wa Jeneva kutofikia muafaka na  ni hatua gani sahihi ichukuliwe kunako mgogoro huo.

Akimalizia kwa kusema: Mwezi March nilichaguliwa kuwa msuluhishi wa Syria, kitu cha kwanza ni niliwataka waasi wa Syria kukabidhi Silaha zao ila maombi yangu hayakutekelezwa hadi sasa hii ni ishara kuwa hakuna ushirikiano hata kidogo hasa kwa upande wa waasi na wanaounga mkono waasi hao.

 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani