Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  

Nuskha za Qur'ani zilizo na makosa zaonyeshwa katika maonyesho ya Algeria
Namba: 271479 Tarehe: 1390/00/00Rejea: iqnaprint

Nuskha za Qur'ani zilizo na makosa zaonyeshwa katika maonyesho ya Algeria

Nuskha za Qur'ani Tukufu zilizo na kasoro za kurasa na aya, zilizopitishwa na Jumuiya ya Utafiti ya al-Azhar zimeonyeshwa katika maonyesho ya 16 ya kimataifa ya vitabu nchini Algeria. 

 Nuskha za Qur
Nuskha za Qur'ani Tukufu zilizo na kasoro za kurasa na aya, zilizopitishwa na Jumuiya ya Utafiti ya al-Azhar zimeonyeshwa katika maonyesho ya 16 ya kimataifa ya vitabu nchini Algeria.

Katika nuskha hizo zaidi ya kurasa 30 na aya 200 za Suratul Baqara zimedondoka kwa maana kwamba kurasa za nne hadi 35 za Qur'ani yaani tokea aya ya 16 hadi 226 za suratul Baqara zimedondoka.

Wageni wanaotembelea maonyesho hayo wamelalamikia vikali suala hilo na kuikosoa kamati inayosimamia maonyesho hayo kwa kuruhusu nuskha hizo za Qur'ani kuonyeshwa kwenye maonyesho hayo.

Maonyesho hayo yaliyoanza tarehe 21 Septemba yakiyajumuisha mashirika ya uchapishaji 512 yakiwemo 376 ya kigeni kutoka nchi 35 za dunia yalimalizika tarehe Mosi Oktoba
 
Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani