Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Mahakama ya Ufaransa yamwachilia huru mhalifu aliyevunjia heshima Qur'ani
Namba: 274400 Tarehe: 1390/00/00Rejea: iqnaprint

Mahakama ya Ufaransa yamwachilia huru mhalifu aliyevunjia heshima Qur'ani

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimeripoti kuwa kesi iliyokuwa ikimkabili Mfaransa mmoja mkazi wa mji wa Strasbourg ambaye alivunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani kwa kukichoma moto na kisha kukikojolea imesikilizwa leo Jumanne, na kutupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa ya mji huo. 

 Mahakama ya Ufaransa yamwachilia huru mhalifu aliyevunjia heshima Qur
Mahakama hiyo imedai kwamba licha ya kuwa picha za video zilizoonyeshwa kupitia mtandao wa intaneti na mhalifu huyo Ernesto Rojas Abbate zilikuwa za kukera na za kichochezi, lakini eti hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kwamba alikusudia kuchochea hisia za ubaguzi, chuki au vitendo vya ghasia dhidi ya Waislamu.
Baada ya mahakama hiyo kutoa hukumu hiyo wakili wa mhalifu huyo mbaguzi amejigamba na kudai kwamba madai ya kukosewa heshima matukufu ya kidini hayapasi kutolewa katika nchi ya kisekula na isiyozingatia mafundisho ya kidini katika uendeshaji wa mambo yake kama vile Ufaransa.
Rojas Abbate alitiwa nguvuni na polisi ya Strsbourg baada ya Waislamu kulalamikia vikali hatua yake ya kuonyesha kitendo hicho kichafu dhidi ya Qur'ani Tukufu katika mkanda wa video. Kitendo hicho cha dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu kilifanywa na mbaguzi huyo mwezi Oktoba mwaka uliopita.
Licha ya kuwa mwendesha mashtaka wa Strasbourg alikuwa ametaka mahakama itoe kifungo kisicho na maana cha mhalifu huyo kusalia nyumbani kwa muda wa miezi mitatu na kutozwa faini ya euro 1000, lakini mahakama ya rufaa imeharibu zaidi mambo kwa kufutilia mbali moja kwa moja mashtaka yaliyokuwa yakimkabili mhalifu huyo
 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani