Ripoti ya ABNA-Baada ya kuongea maneno ya kumdhalilisha Mtume(saw) Mufti ya Saudia Arabia Muhammad Al arifiy aliomba msamaha baada ya kuongea maneno ya kumdhalilisha Mtume(saw) na kueleza; baada ya kurejea maneno yangu yasokuwa na msingi ya kumdhalilisha Mtume(saw) naomba msamaha na kutubu kwa Mwenyezi Mungu kwa maneno yangu na kusisitiza kuwa Masunni wanamheshimu Mtume Muhammad(saw). Dr.Jamil Al lawiq Mwalimu wa Sheria wa Chuo cha Ta`aif:Maneno yasokua na uhakika ndani yake na kuongea maneno usokua na elimu nayo ikiwa yatasababisha madhara katika Dini na Itikadi zake ni kosa na ni Dhambi kubwa kwa mwenye kuzungumza maneno hayo. Muhammad A`ali Zulfah Mbunge Mstafu wa Saudia alisema:Maneno kama haya yanaleta madhara katika Uislam hasa kwa Waislamu wa kawaida wasokua na elimu ya Dini husababisha kupotea njia na kuwa na muelekeo usofahamika katika Uislamu, hii ni hatari katika Uislamu. Mufti wa Saudia Arabia kabla ya Toba yake alieleza kwa kusema; Mtume Kabla ya kubla kuharamishwa Pombe alikuwa akinywa Pombe na kuwapa watu zawadi ya Pombe na kuitikadi kuwa Pombe si Najisi, ila maneno hayo yalikutwa upinzani mkali wa vyombo vya habari vya nje mwa Saudia, lakustaajabisha ni kwamba Nchi ya Saudia ilikaa kimwa na kufumbia macho suala hilo. Gazeti la Saudia Arabia’Jaza`an’ lilieleza kuwa; Chmbo cha habari cha kwanza kilichozungumzia suala hili ni AL ALAM ambayo ni Televisheni ya Iran, ili laani vikali maneno hayo na kueleza kuwa maneno hayo ni kumdhalilisha Mtume(saw). Baada ya kuongea maneno hayo Muakilishi wa Mashia wa Kuwait Ayatullah Sayyid Muhammad Baqir Al mahriy alisema: Maneno ya Al arifiy ni kumdhalilisha Mtume Muhammad(saw) na kuzuiya uwongo, na madai ya kuwa Pombe si Najisi ni maneno yasokuwa na mantiki kwani Qurani Tukufu kunako Pombe imeweka wazi kabisa kueleza kuwa Pombe ni Najisi na ni haramu kunwewa, Surat Al Maidah Aya ya 90 imeweka wazi kila kitu. Mufti wa Kiwahabi wa Saudia Arabia baada ya kujirejea na kurejea maneno kwa kumdhalilisha Mtukufu Mtume Muhammad(saw) na alitubu kwa Mwenyezi Mungu kwa kosa alofanya na kuomba msahama Waislamu wote kwa kosa hilo.