Ripoti ya ABNA-Sheikh Ahmad Kabisiy Mufti wa Kisunni katika maongezi yake na Televisheni ya Dubai 1 alisema:Muawiyah na Baba yake Abu Sufiani ndio wasababishaji wa matatizo ya Ulimwengu wa Kiislamu.
Alikiashiria kwa kusema; kutetea Kundi la Kiwahabi shakhsia ya Muawiyah na kusahau nini alifanya enzi za Imam Ali Ibn Abi Talib kumlaani katika kila Swala ya Ijumaa.
Mufti huyu wa Kisunni alisisitiza kusema naapa kwa jina la Mungu kila aina ya matatizo yanayo tusibu chanzo chake ni hao watu wawili, kueleza kua hakuna tufauti baina ya Shia na Sunni.
Sheikh Ahmad Kabisiy katika kipindi cha Televisheni hiyo alijibu Swali la Mtazamaji wa kipindi hicho akiulizwa, kati ya Ali Ibn Abi Talib na Muawiyah afatwe nani?! Alisema: kuwa mfasi wa Ali Ibn Abi Talib na umuombe Mungu akufufue nae.
Baada ya kipindi hicho cha Televisheni Mawahabi wa Nchi ya Emirat waliandamana na kuomba kutolewa Sheikh Ahmad Al kabisiy.
Sheikh Ahmad kabisiy asili yake ni Muiraq anaeishi Nchi ya Emirat na ni Mufti wa Kisunni katika Mji wa Dubai.