| Namba: 306951 | Tarehe: 2012/04/07 - 10:21 | Rejea: ABNA.ir | print |
Muamko wa Kiislamu Mauaji ya kinyama kuendelea Bahrain |
Ripoti ya ABNA- Kwa mara nyingine tena leo asubuhi aliuawa Mama mmoja wa Kibahrain, na habari zinaeleza kuwa athari ya kifo chake ni Gesi ya sumu inayotumiwa na Polisi wa Nchi hiyo wakishirikiana na Saudia Arabia.
Khadija Muhammad Ali A`ali Ab bas mwenye umri wa miaka 49 alifariki baada ya kuumwa miezi mitatu, na sababu ya kifo chake ilielezwa baada ya kukagua maiti yake na kuonekana sababu ya kifo chake ni athari ya Gesi ya sumu inayotumiwa na Polisi wa Nchi hiyo kushirikiana na Saudia Arabia.
Mama huyu katika miezi mitatu hiyo alitaabika na maradhi yasojulikana na kila tiba ilikuwa haina faida hatimae alikubali wito wa Mwenyezi Mungu na kufa kishujaa baada ya kuonyesha msimamo wake dhidi ya utawala wa Kifalme wa Bahrain unaosaidiwa na Saudia Arabia kukandamiza Wananchi.
Shahada ya Mama huyu iliongeza idadi ya Mashahidi wa Bahrain kufikia watu 83 wa muamko wa Kiislamu.