| Namba: 307173 | Tarehe: 2012/04/08 - 09:55 | Rejea: abna.ir | print |
Waandishi wa habari wa Al jazeerah Baada ya kujiuzulu atowa siri za Al jazeerah |
Ripoti ya ABNA- NTV Televisheni ya habari ya Kituruki imeeleza, kutonana na habari za uongo zinazotangazwa na Televisheni ya Al jazeerah watangazaji wa Tano wa Televisheni hiyo walijiuzulu na kutoa siri za Al jazeerah, NTV habari hiyo iliipa anuani ya ‘Zilzala ya Syria kuikumba Al jazeerah’
Ripoti hiyo inaeleza; Waandishi wa habari wa Al jazeerah kazi yao ni kufuata na kusambaza habari za uongo kunako Syria na kutoeleza uhakika wa mambo jinsi ulivyo.
Kwa sababu hiyo watangazaji wa Tano wa Televisheni hiyo walijiuzulu baada ya kulazimishwa kutangaza habari za uongo kunako Syria, miongoni mwao ni; Aliy Al hashimiy, Ahmad Musa na Khalid Abu Sala`ah.
Alisema Aliy Al hashimiy: Miezi mitano ilopita nililazimishwa kutangaza habari ya uongo kuvamia Syria Lebanon na kurushwa kombora kadhaa mipakani mwa Lebanon, habari hii niliikanusha na kuipinga ila Al jazeerah walinilazimisha kuitamgaza na kuwa sababu ya kujiuzulu kwangu.
Ahmad Musa: Habari zinazoelezwa kunako Syria na Lebanon ni propaganda na hazina ukweli ndani yake hasa habari zinazo husu Syria ni habari za sehemu nyengine na kuelezwa kuwa ni matokeo na vurugu za Syria, mimi ni mmoja kati ya walokua wakifanya kazi hizo.
Khalid Abu Sala`ah: Habari zinazoeleza kuwa Serikali ya Syria inauwa Watoto si kweli!, wanaofanya hayo ni waasi hurusha makombora na kueleza kuwa ni Serikali ya Syria ndio yafanya hayo, mimi ni mmoja katika waloagizwa Mkoa wa Hims na kutangaza habari za uongo kunako serikali ya Syria.
Watangazaji wengine pia walisisitiza maneno hayo na kuunga mkono kuwa yanayofanyika Syria si serikali ya Syria bali ni waasi ndio wa haribifu na watendaji wa mambo hayo.