| Namba: 310290 | Tarehe: 2012/04/22 - 10:15 | Rejea: | print |
Uchaguzi wa Rais wa Ufaransa kuanza leo |
Utabiri wa kiwango cha juu na kura ya nguvu ya upinzani umeyaacha matokeo yakiwa hayatabiriki lakini kura zote za maoni zinaelekeza kwa mpinzani wa rais Sarkozy wa chama cha soshalist Franswaa Hollande.Wakongwe hao wawili wa siasa wapo katika hatua za kukabiliana uso kwa uso katika duru la pili la uchaguzi May 6 uchaguzi ambao utaamua nani ataliongoza taifa hilo ambalo linatajwa kuwa taifa la tano lenye nguvu duniani katika miaka mitano ijayo.