| Namba: 316331 | Tarehe: 2012/05/20 - 05:17 | Rejea: ABNA.ir | print |
Mkutano wa kundi la nchi 8 wafunguliwa rasmi |
Obama ili kuvutia Nchi za Afrika na kujitoa kimasomaso ametangaza mpango wa kutoa dola za kimarekani milioni
3 kwa sekta binafsi kwa ajili ya usalama wa chakula na uzalishaji wa kilimo
katika nchi za Afrika, na kuzitaka nchi nyingine wajumbe kutekeleza sehemu yao.
Aidha amesema mataifa ya kundi la nchi hizo yana maadili, uchumi na usalama
mkubwa wa kuongoza mapambano dhidi ya njaa na utapiamlo katika Afrika, licha ya
kwamba nchi hizo zinakabiliana na changamoto ikiwemo kutoa ajira, hali ya nchi
zinazotumia euro na kurejesha hali ya uchumi wa dunia.