Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Palestina yachukizwa na kauli ya mgombea kiti cha urais nchini Marekani Mitt Romney
Namba: 333464 Tarehe: 2012/08/01 - 02:55Rejea: ABNA.irprint

Palestina yachukizwa na kauli ya mgombea kiti cha urais nchini Marekani Mitt Romney

Serikali ya Mamlaka ya Palestina imechukizwa na kauli ambayo ameitoa Mgombea Mtarajiwa wa Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Republican nchini Marekani Mitt Romney dhidi ya taifa hilo wakiamini ni yenye lengo la kueneza chuki.

 

 Palestina yachukizwa na kauli ya mgombea kiti cha urais nchini Marekani Mitt Romney

Mpatanishi Mkuu wa Serikali ya Mamlaka ya Palestina Saeb Erakat amemjia juu Romney ambaye alikuwa nchini Israel na kusema matamshi yake ya kuona serikali ya Jerusalem ni bora kuliko yao ni kitu kibaya sana.

Erakat amekwenda mbali na kuweka bayana matamshi kama haya hayawezi kusaidia mchakato wa kupatikana kwa amani katika eneo la Mashariki ya Kati kama ambavyo juhudi zimekuwa zikifanywa.

Upande mwingine Mgombea huyo mtarajiwa wa Urais kupitia Tiketi ya Chama Cha Repuclican nchini Marekani Mitt Romney amewasili nchini Poland kuendelea na ziara yake katika mataifaya Ulaya huku akitumia sehemu kubwa ya hutoba yake kusifia uchumi wa Taifa hilo.

Romney bila ya wasiwasi wowote amepongeza kwa kiasi kikubwa juhudi ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Viongozi wa Poland katika kuhakikisha uchumi wao unaimarika tangu mwaka jana.

Mgombea huyo Mtarajiwa wa kiti cha urais amekuwa kwenye ziara ambayo inatafsiriwa kama ya kusaka uungwaji mkono na hapa akapata fursa ya kuhutubia wananchi wa Poland waliojitokeza kumsikiliza.

 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani