| Namba: 337696 | Tarehe: 2012/08/18 - 12:45 | Rejea: abna | print |
Siku ya kimataifa ya Qudsi nchini Sudani |
Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani Imam khomein(r.z) ameipa jina siku hiyo kuwa ni siku ya kimataifa ya Qudsi, kwaajili hiyo makhatibu wengi duniani katika siku hiyo huipa kipaumbele hutuba zao za ijumaa kuizungumzia siku hiyo ya Qudsi, miungoni mwa nchi zilizo adhimisha siku hiyo ni nchi ya Sudani katika mikoa tofauti ya nchi hiyo
Hujatul Islamu malakutiy, mkuu wa kitengo cha tamaduni nchini humo naye kwa manasaba huo wa siku Quds alihudhuria katika msikiti wa Shahidi katika mkoa wa Khartom na baada ya hutuba ya sala ya ijumaa alizungumzia kuhusu siku hiyo.
Kabla ya mazungumzo ya malakutiy, Sheikh Muhammad Hasan Tanun, hatibu wa sala ya ijumaa, katika hutuba yake ya kwanza na yapili alizungumzia siku ya kimataifa ya Qudsi, nakuwataka waislamu wote kutafakari kuhusu waislamu wenzao wapalestina ambao waloharamishiwa haki za kibinadamu, wananchi ambao wako katika dhulma na makucha ya wazayuni, waislamu ambao ibada zao za kila siku hawazifanyi kwa uhuru na amani,
Aidha aliwataka wasudani wote kufanya hima katika kuwasaidia wapalestina,hasa katika siku ya Qudsi kuwasaidia waislamu kwa mali na ghali kuhakikisha inakombolewa palestina na masjidil Aqswa takatifu.
Na baada ya sala hiyo ya ijumaa Imam wa msikiti huo alimkaribiasha Hujatul Islam Malakutiy, naye malakutiy baada ya shukurani alitanguliza kusoma Hadithi ya mtume (s.a.w.w) isemayo:mwenye kuamka asubuhi haliyakuwa ayatilii umuhimu mambo yanayowasibu waislamu basi mtu huyo si muislamu.
Naye aliendelea kusema Imam Khomein mwanzoni mwa mapinduzi ya kiislamu ya Iran aliwataka wanadamu duniani kuwasaidia wapalestina na kuitangaza ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa nisiku ya kimataifa ya Qudsi na kuyataka mataifa yote kuwanusuru waislamu hao
.