Abna.ir


Iran yaionya Marekani kwa kuweka ndege zake katika Umoja wa Falme za Kiarabu
Iran yaionya Marekani kwa kuweka ndege zake katika Umoja wa Falme za Kiarabu

Waziri wa ulinzi wa Iran amesema hatua ya Marekani ya kuziweka ndege za kivita aina ya stealth katika Umoja wa Falme za Kiarabu itavuruga usalama wa eneo.

Kauli ya waziri huyo Jenerali Ahmad Vahidi ndiyo msimamo rasmi wa kwanza juu ya taarifa za vyombo vya habari kuhusu hatua ya Marekani ya kuziweka ndege zake za kivita aina ya F22 kwenye kituo cha anga cha Al Dafra cha Umoja wa Falme za Kiarabu. Ndege za Marekani zimekuwapo kwenye kituo hicho kwa muda mrefu. Waziri wa ulinzi wa Iran amesema kuwekwa ndege hizo ni kampeni ya kisaikolojia. Ameeleza kwamba usalama unapaswa kuhakikishwa na nchi za eneo husika. 


http://www.abna.ir/data.asp?lang=17&id=312244