Abna.ir


Sarkozy kuangushwa chini
Athari za muamko wa Kiislamu
Sarkozy kuangushwa chini

Chana cha mrengo wa kulia kushindwa uchaguzi wa urais Ufaransa baada ya miaka 17, sababu yake ni kuiga msimamo walokuwa nao Waislamu, kuiga kile kinacho tokea katika Nchi za Kiislamu kama Misri, Libya, Bahrain, Yemen, Tunisia na Saudia Arabia, yote hhayo ni kuonyesha Ulimwengu kuwa Wafaransa nao waweza leta mageuzi na mabadiliko ya Nchi yao.

Bw Francois Hollande amechaguliwa kuwa rais wa Ufaransa baada ya kumshinda mpinzani wake ambaye ni rais wa sasa Bw Nicolas Sarkozy, katika duru ya pili ya upigaji kura ya uchaguzi mkuu iliyofanyika siku ya Jumapili. Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa na wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa, Bw Hollande mgombea kutoka chama cha mrengo wa kushoto amepata asilimia 51.24 ya kura huku Bw Sarkozy wa chama cha mrengo wa kulia akipata asilimia 48.76 ya kura. Ushindi wa Bw Hollande umemaliza hali ya watu wa mrengo wa kulia kuhodhi nafasi ya urais katika miaka 17 iliyopita.


http://www.abna.ir/data.asp?lang=17&id=313828